Tume ya uchaguzi nchini Burundi imesema kuwa itatangaza matokeo ya kura ya maoni baadaye hii leo iliyopigwa hivi karibuni.
Kiongozi wa upinzani nchini humo, Agathon Rwasa amesema kuwa hatokubali matokeo ambayo yatatagazwa akitaja kuwa kura hiyo iligubikwa na udanganyifu mkubwa na vitisho kwa wafuasi wake.
Rwasa ameitaka tume ya uchaguzi kufuta matokeo hayo na kutangaza upya upigaji wa kura ya maoni nchini humo ili kila mtu ashiriki akiwa huru.
Aidha, iwapo katiba hiyo itaidhinishwa, itamruhusu Rais Pierre Nkurunzinza kuwania tena uongozi na kuitawala nchi hiyo hadi mwaka 2034.
Hata hivyo, risala iliyowasilishwa kwenye tume ya Uchaguzi, Agathon Rwasa na kambi yake ya Muungano wa Amizero y’Abarundi au Matumaini ya Warundi wamesema kura ya maoni haikuwa huru wala ya uwazi na haki.