Zifuatazo ni baadhi ya nukuu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa wakati wa hafla ya utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma Oktoba 22, 2023..

“ukweli ni kuwa sisi sio mlango Bahari pekee Mashariki na Kusini mwa Afrika, kuna milango Bahari mitatu ambayo ni Mombasa, Beira na Durban lakini upande wa Magharibi kuna milango ya Bahari ya Walvis Bay na Lobito.”

Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Godius Kahyarara wakitia saini Mkataba wa Nchi Mwenyeji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyowakilishwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma Oktoba22, 2023.

“Maana yake ni kwamba wanaotaka mizigo yao ifike, wanauwezo wa kuchagua Bandari yoyote wakaitumia. Kinachotupa sisi turufu dhidi ya washindani wetu ni bahati ya Mlango Bahari wetu kuwa na masafa mafupi kuingia nchi za Jirani na tunafikika na nchi nyingi kwa kutumia mpaka mmoja tu ikilinganishwa na milango bahari mingine.”

Ameongeza kuwa, “ukaribu pekee sio hoja ya kutosha, hivyo ni muhimu kuangalia ufanisi kwani wafanyabiashara hutazama pia ufanisi na gharama.

Dkt. Samia: Niwape uhakika maslahi ya nchi yamelindwa
Kumbukizi ya Nyerere yamalizia ujenzi Kambarage