Wiki moja baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu na msimamizi wa Uchaguzi huo kumtangaza kada wa Chadema, Tundu Lissu kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Singida Mashariki akikitea nafasi hiyo, aliyekuwa mgombea kupitia CCM, Jonathan Njau amepinga matokeo hayo.

Njau amemtuhumu Tundu Lissu na msimamizi wa kituo hicho kwa kufanya udanganyifu na amechukua uamuzi wa kumuandikia barua msimamizi wa uchauguzi huo, Mohammed Nkya akihoji na kupinga matokeo hayo.

Njau alidai kuwa kuna udanganyifu uliofanyika na kusababisha matokeo ya uchauguzi huo kukinzana.

“Huu ndio mtiririko, mule ndani ya mabox kuna paka ama kuna panya?” Kwa sababu kama anaweza kutuambia yote haya. Yote ni ya uongo yanakinzana na hakufuata utaratibu. Tumemuomba aturuhusu tufanye majumuisho upya,” alisema Njau.

Hata hivyo, Msimamizi huyo aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki na kumtaka yoyote mwenye malalamiko kuyafikisha mahakamani.

Hii itakuwa mara ya pili Njau ambaye ni mwanasheria kufikisha mahakamani malalamiko yake dhidi ya ushindi wa Tundu Lissu. Mwaka 2010, Njau ambaye alishindana na Lissu kukalia kiti cha uwakilishi cha jimbo hilo alitimkia mahakamani baada ya msimamizi kumtangaza Tundu Lissu kuwa mshindi. Hata hivyo, Lissu alishinda kesi hiyo.

 

Sikio la Baba Na Mama Izzo Bizness ni Chanzo cha Tunayoyasikia
Kafulila: Sikuibiwa Kura, Nilinyang’anywa Ushindi Kwa Nguvu