Rapa toka Mbeya, Izzo Bizness ameeleza moja kati ya vitu ambavyo watanzania wengi hawavifahamu kuhusu nyimbo zake tunazoziskia, huku akiwataa wazazi wake kama chujio la kwanza la maamuzi ya nyimbo zake.

Izzo ameeleza kuwa kila anapomaliza kufanya wimbo anaotaka kuufikisha kwenye kiwanda cha muziki, huwasikilizisha kwanza wazazi wake ambao hufanya machaguo na kumshauri kabla hajamsikilizisha mtu yoyote. Hivyo, endapo wazazi wake hawatapenda midundo na michano kwenye ngoma hizo, mashabiki hawatausikia wimbo huo au utafanyiwa marekebisho kwanza.

Izzo Bizness

“Watu wengi tumezoea unaweza kwenda kumsikilizisha kwanza promota ama radio presenter mwanzoni ama watu wako wa karibu nyumbani na nini. Lakini mimi huwa nawasikilizisha wazazi wangu kwa sababu ni watu ambao wananisapoti kwa hiki ninachokifanya, kwa hiyo kuwa nawahusisha wao halafu ndio nakuja kwa akina fulani na fulani,” alisema Izzo Bizness.

 

Kukamatwa Watumishi Kituo Cha Sheria Na Haki Za Binadamu Kwazua Utata
Ushindi wa Tundu Lissu Wazua Utata