Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba amesema kuwa alikuwa akipigania sana swala la madini kwenda sokoni mwaka 2015 ambapo biashara ya dhahabu na madini yote ilikuwa ni haramu kwani Serikali ilikuwa haichukui ushuru.

Kishimba ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media na kueleza kuwa Serikali ni vyema Serikali kuweka mipango thabiti ya uchukuaji wa ushuru kwenye dhahabu kwa lengo la kukuza uchumi wa wancanchi na pato la Taifa.

Amesema, ”mimi ndiye mbunge pekee ambaye nilisema serikali lazima ichukue ushuru kwenye dhahabu ama mnunue, kwasababu hii dhahabu hata mkikataa inaenda ulaya mwisho wa yote tena nyinyi mnaomba hela ulaya wanakata dhahabu hiyo wanawapa nyie sasa nyie mnasema haramu.”

Aidha, Kishimba ameongeza kuwa ”lakini bahati nzuri baada ya mvutano mkubwa baadaye Hayati Magufulia  alielewa na sasa masoko ya dhahabu na madini yakawa yametoka manake unajua watu wote walikuwa wanaamini madini labda ni kitu kibaya na wazungu walikuwa wameshatuaminisha hivyo.”

Hii hapa tafsiri halisi ya neno Katerero
Sadio Kanoute kimeeleweka Simba SC