Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema suala la utatuzi wa changamoto za Muungano halijakwama wala halijasuasua.
Khamis Hamza ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Same Magharibi Dkt. David Mathayo David aliyetaka kujua ni changamoto zipi za Muungano zimetatuliwa na zipi zimebaki.
Amesema hadi sasa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), zimejadili na kuzipatia ufumbuzi jumla ya changamoto 22 zikiwemo Gharama za Kushusha Mizigo Bandari ya Dar es Salaam kwa Mizigo inayotoka Zanzibar na Utafutaji na
Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia.
Akiendelea kujibu swali hilo amesema kuwa Hoja zilizobakia kutatuliwa ni nne ambazo ni Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Usajili wa Vyombo vya Moto, Uingizaji wa Sukari katika Soko la Tanzania Bara na Mgawanyo wa Mapato Yatokanayo na Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na Faida ya Benki Kuu.
Hata hivyo, amesema Hoja nne zinazoendelea kutafutiwa ufumbuzi ni pamoja na Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya Fedha, Usajili wa Vyombo vya Moto, Uingizaji wa Sukari katika Soko la Tanzania Bara na Mgawanyo wa Mapato Yatokanayo na Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki
na Faida ya Benki Kuu.