Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan amemuonya rais wa Urusu, Vladimir Putin kutocheza na moto kuhusu suala la jeshi lake kuidungua ndege ya Urusi Jumanne wiki hii.

Rais Erdogan alitoa onyo hilo wakati alipokuwa akilihutubia taifa lake kwa njia ya Televisheni. Aliongeza kuwa anataka kuoanana uso kwa uso na Putin ili wajadili suala hilo na kutafuta namna ya kuumaliza mzozo huo.

Hata hivyo, rais Putin aliweka msisitizo wake kuwa anataka Uturuki iombe radhi kuhusu tukio hilo kabla hajakutana na Erdogan.

Rais Erdogan na Rais Putin

Taarifa zilizotolewa na msaidizi wa rais Putin zimeeleza kuwa nchi Urusi imesitisha mpango wa raia wa nchi hizo kusafiri kati ya nchi hizo bila kuwa na Visa, hadi pale hatua stahiki zitakapochukuliwa.

Uturuki imeendelea kusisitiza kuwa ndege ya kijeshi ya Urusi iliruka katika anga yake na kupuuza ishara za ya tahadhari waliyopewa. Hata hivyo, Urusi nayo imeendelea kusisitiza kuwa ndege hiyo ilikuwa katika anga ya Syria.

Video: Boss Wa Empire Alazimika Kuelezea Kitendo Cha Jamal (Shoga) 'Kum-Kiss' Msichana
Timu Ya Taifa Ya Vijana Yaingia Kambini