Kitendo cha muigizaji nyota wa Series maarufu ya Empire, Jussie Smollet (Jamal) ambaye anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga) na akiwa amejitangaza hadharani, kumbusu kwa hisia mrembo Skye kimezua zogo na mshangao kwa mashabiki.

Jamal aliwasuprise mashabiki baada ya kumbusu Skye kwa hisia kali, kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokea katika maisha yote ya filamu hiyo kutokana na hali ya Jamal. Mashabiki hao walimwaga hisia zao kupitia mtandao wa Twitter.

Wengi walihoji kama shoga anaweza kuwa na hisia za kuvutiwa na msichana mrembo au imetokea vipi katika maisha ya Jamal.

Mshituko huo wa mashabiki ulimlazimu Boss wa Empire, Ilene Chaiken kutoa ufafanuzi.

“Tunafahamu wazi kwamba Jamal ni shoga na yeye ameweka wazi hilo, lakini ilitokea tu. Ni katika hali ya kuigiza kitu fulani na kukibeba na kutokielezea au kukitafakari,” alisema.

Alisema kuwa kuweka kipande hicho kulitokana na uamuzi wa muongozaji aliyetaka kufanya kitu cha kuwashtua watazamaji na kwamba alifanikiwa kufanya hivyo.

Chaiken aliongeza kuwa mashabiki wategemee kuendelea kupata mshangao kwenye episode ya 10 na nyingine za Msimu huo wa Pili.

 

Mo Dewj ashinda tuzo ya Forbes, amshinda Rais wa Nigeria
Uturuki Yaionya Urusi ‘Kutocheza na Moto’ Baada ya Kuidungua Ndege yake