Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limeuteua uwanja wa Millennium uliopo mjini Cardiff nchini Wales kutumika kwa ajili ya mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2017.

Kamati kuu ya shirikisho hilo imefikia makuabaliano ya kuuteua uwanja huo baada ya kuona unakidhi vigezo vinavyostahili kuhodhi mchezo mkubwa wa fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Uwanja huo ambao unamilikiwa na chama cha mchezo wa Rugby nchini Wales, ulifunguliwa rasmi mwaka 1999 na ulikua unatumika sana kwa ajili ya michezo ya hatua ya fainli ya kombe la chama cha soka nchini England FA, kuanzia mwaka 2001 mpaka mwaka 2006.

Uwanja huo pia ulitumiwa na FA kwa ajili ya michuano ya kombe la ligi pamoja na mchezo wa ngao jamii, baada ya kuvunjwa kwa uwanja wa Wembley.

Una uwezo wa kuchukua mashabiki walioketi 74,500 na ulitumika wakati wa michuano ya Olympic ya mwaka 2012.

Katika hatua nyingine kamati kuu ya UEFA, imeuteua uwanja wa Friends Arena uliopo mjini Stockholm nchini Sweden kwa ajili ya mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya Europa League mwaka 2017.

Picha: Chris Brown aonesha jumba jipya na tattoo mpya
Matola Ataja Waliopendekeza Usajili Wa Kiiza Simba
Tags