Shirikisho la soka nchini Uholanzi limemteua tena Louis van Gaal kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa hilo kwa kandarasi mwaka mmoja ambayo itafikia kikomo mwishoni mwa mwaka wa 2022.

Van Gaal anachukua jukumu la kukiongoza kikosi cha Uholanzi kwa mara ya tatu, ambapo awali alikuwa alikiongoza kuanzia mwaka 2000 hadi 2001 na kisha mwaka 2012 hadi 2014.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 69 atasimamia jukumu la kuhakikisha kikosi cha Uholanzi kinafuzu Fainali za Kombe la Dunia la 2022, na kandarasi yake itaendelea hadi mwisho wa Fainali hizo zitakzounguruma nchini Qatar kwa mara ya kwanza.

Van Gaal aliwahi kustaafu shughuli za ukocha, kwa kigezo cha kupata msukumo kutoka kwenye familia yake, lakini kurejea tena kazini kunadhihirisha bado anaipenda kazi hiyo ambayo ameifanya akiwa kama mchezaji na kisha mkuu wa benchi la ufundi.

Maamuzi ya Shirikisho la Soka nchini Uholanzi ya kumkabidhi kikosi meneja huyo wa zamani wa klabu za Man Utd, FC Bayern Munich na Ajax Amsterdam yametokana na kuondoka kwa Frank de Boer.

De Boer, aliachana Uholanzi, baada ya ‘The Orange’ kushindwa kufurukuta kwenye Fainali za EURO 2020 zilizomalizika mwezi Julai jijini London kwa Italia kuwa Mabingwa.

Uholanzi iliondolewa kwenye Fainali za Euro 2020 katika hatua ya mtoano (16 Bora).

Rais Samia akutana na Naibu Waziri mambo ya Nje wa Marekani
RC Makalla akemea Urasimu na Rushwa