Boss wa Young Money Entertainment, Lil Wayne alikatika mzuka wa kuendelea kutema mistari jukwaani baada ya mashabiki wa jiji la Milani nchini Italia kumuangalia akitumbuiza kama wanaangalia tamthilia ya Kikorea.

Kwa mujibu wa TMZ, Lil Wayne aliwaambia mara kadhaa mashabiki kunyoosha mikono juu lakini mashabiki hao hawakufanya hivyo hali iliyompa gadhabu na kuamua kuwarushia kikuza sauti (microphone) na kuondoka jukwaani kabla show yake haijaisha.

Why #lilwayne acting like this at these people fashion show? ? part 2 of 2

A video posted by Baller Alert (@balleralert) on

Hata hivyo, muwakilishi wa rapa huyo alieleza kuwa hakutupa microphone kwa sababu ya mashabiki bali alifanya hivyo kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyokuwa kwenye ukumbi huo ikiwa ni pamoja na mic hiyo kutotoa sauti vizuri.

 

Anthony Diallo: TCRA wanatuchafulia jina
Polisi yawasaka wamiliki na wahariri wa Gazeti la 'Mawio'