Mmiliki wa Sahara Media Group, inayomiliki vituo vya Star TV, Radio Free Africa na Kiss Fm, Anthony Diallo amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewachafulia jina kwa kutoa taarifa kwa umma ya kuwafungia bila kuwataarifu kwanza wahusika.

Diallo ameyasema hayo ikiwa ni saa chache baada ya TCRA kupitia Meneja wake wa Mawasiliano,Innocent Mungi kutaja orodha ya vituo vya redio na TV vilivyofungiwa kutokana na kutolipa tozo na ada kwa mujibu wa sheria, huku vituo vinavyomilikiwa na Sahara Media Group vikitajwa pia.

“Hatujapata taarifa rasmi, kama wameita waandishi wa habari wakazungumza nao bila kuwaambia wahusika ambao ni sisi… wanatuchafulia jina ilihali matatizo ya msingi hawajamaliza,” Diallo aliliambia Mwananchi.

Aliongeza kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na TCRA walimlalamikia kuhusu kuwapa ankara ya malipo kwa dola badala ya shingili za Tanzania.

Hata hivyo, Mungi alikanusha maelezo ya Diallo na kudai kuwa kila kampuni ilipelekewa taarifa na wahusika walisaini kuzipata.

Alisisitiza kuwa vituo vilivyotajwa vitaendelea kurusha matangazo lakini ifikapo saa sita wa leo vitafungiwa kurusha matangazo lakini atakayelipa ada na tozo hizo kabla ya muda huo ataendelea kubaki hewani.

Bavicha wataka Msajili aifute CCM, la Sivyo watafanya hili
Video: Lil Wayne awarushia 'microphone' mashabiki walioshindwa kumshangilia