Takribani watu tisa wamejeruhiwa na majambazi baada ya kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia mgodi wa dhahabu uliyopo katika kijiji cha Nyakivangala, Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa.
 
Mbali na kujeruhi, majambazi hao wamepora zaidi ya Shilingi Milioni 81, dhahabu zaidi ya gramu 400, na baadhi ya mali za wafanyabiashara katika eneo hilo.
 
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya hiyo, Richard Kasesela amesema tukio hilo lililitokea majira ya saa nne usiku.
 
Kasesela amesema kuwa Jeshi la Polisi linasaka majambazi hao huku akieleza kuwa Serikali inashirikiana na wananchi wa eneo hilo kuhakikisha kituo cha Polisi kinajengwa ili kuimarisha usalama wa wananchi katika maeneo hayo.
 
Aidha, amewataka watu wanaofanya shughuli zao katika maeneo hayo kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kutokutembea na kiasi kikubwa cha fedha kwani sasa teknolojia imekuwa hivyo wanaweza kuhifadhi pesa zao hata kupitia mitandao ya simu.

Video: Meya, Mkurugenzi wapewa siku moja kutoa maamuzi ya kiwanja
Bosi EWURA atumbuliwa