Kundi la muziki la Major Lazer lenye makazi yake Los Angeles nchini Marekani wiki hii limeachia video ya wimbo mpya ‘All My Life’, wakimpa shavu Burna Boy wa Nigeria.

Ngoma hiyo imetoka sambamba na video iliyofanyika jijini Lagos nchini Nigeria chini ya muongozaji  kutoka Afrika Kusini, Adriaan Louw.

Aidha, Major Lazer wamedhamiria kuifanya Afrika ipige shangwe la furaha ya muziki mzuri, kwani wamepanga kufanya ziara katika nchi sita za Afrika ikiwa ni pamoja na nchi mbili za Afrika Mashariki.

Oktoba 6, Major Lazer watakuwa jijini Nairobi nchini Kenya na siku inayofuata watahamia Addis Ababa nchini Ethiopia. Jiji la Kampala litakuwa na ugeni wa Major Lazer Oktoba 8 mwaka huu.

Kabla ya kuzuru majiji hayo, kundi hilo litaanza ziara yake katika jiji ya Johannesburg, Afrika Kusini (Septemba 29) na baadaye Leopards Bay, Malawi.

Kupitia ziara hiyo, watafanya kazi ya kuhamasisha utokomezaji wa ujangili dhidi ya tembo, wakishirikiana na taasisi ya VETPAW (Veterans Empowered to Protect African Wildlife) inayojishughulisha na uhamasishaji wa uhifadhi na ulinzi wa wanyama pori barani Afrika.

Kikosi cha Simba chawasili salama jijini Mwanza
Nafasi za ajira kutoka makampuni 10 Tanzania