Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta amewataka watendaji kuwa wabunifu ili waweze kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam kwenye semina ya siku mbili iliyowakutanisha wenyeviti na watendaji kwaajili ya mafunzo ya utendaji kazi na utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema kuwa kama watendaji hao na wenyeviti watapatiwa mafunzo hayo basi yatachangia kwa kiasi kikubwa kuweza kutatua migogoro inayowakabili wananchi hivyo kuondokana na changamoto zinazowakabili.

“Watendaji hawa na wenyeviti baada ya mafunzo haya watasaidia pakubwa sana kutatua kero ambazo si za lazima, hivyo baada ya mafunzo haya ya siku mbili tutawapa muda wao nao watueleze changamoto zinazowakabili,”amesema Sitta

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 11, 2017
Korea Kaskazini yaiba mafaili ya jeshi la Korea Kusini - Marekani