Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia mjema amefanya ziara katika Kata ya Pugu na Gongo la Mboto jijini Dar es salaam na kusikiliza kero mbali mbali za Wananchi na Wafanyabiashara katika maeneo hayo.

Katika mkutano huo Mjema amechukua hatua mbali mbali kufuatia kero walizotoa wananchi na wafanyabiashara hao, ambapo ameipa Halmashauri muda wa miezi mitatu kurekebisha utaratibu wa ukusanyaji ushuru wa biashara katika soko jipya la Pugu, Kigogo Fresh hivyo kwa kipindi chote hicho ametoa marufuku kukusanya fedha katika soko hilo mpaka miundombinu itakapokuwa sawa.

Wananchi pia wameitaja kero yao kubwa kuwa ni kuhusu Mwenyekiti wa Kata hiyo, Bakari Shingo ambaye hatoi ushirikiano kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuwatolea lugha chafu, kutoweka wazi hesabu za mapato na matumizi, hivyo Mjema ametangaza kuitisha mkutano mwingine  katika Kata hiyo ili kubaini ukweli na hatua zichukuliwe. Bofya hapa kutazama video

Waziri Mkuu anaswa akicheza ‘game’ kwenye simu bungeni mjadala ukiendelea
Vifaa vya kuhakiki vyeti feki vyaibwa