Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Augustino Lyatonga Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), amewashangaa wanaopinga serikali kuhamia Dodoma na kusema kuwa suala hilo lilikuwepo tangu enzi za baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mrema amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na dar24.com leo Septemba 14, 2016 na kumpongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa udhubutu alioufanya kwa kuchukua maamuzi hayo.

“Rais wetu ni mtu makini sana ambaye anatekeleza kile wananchi wanastahili kukipata na si porojo zinazofanywa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya nchi’’- Mrema

Bodi ya Filamu kutoa ushirikiano uanzishwaji wa Mradi wa TYEEO
Serikali Yashauliwa Kutumia Wataalamu Wa Jiolojia Katika Shughuli Za Ujenzi