Mrembo kutoka Miss Tanzania aliyechaguliwa kuiwakilisha nchi katika shindano la urembo Afrika ambalo linatarajia kufanyika Novemba 28, 2016 nchini Nigeria, Julietha Kabete amesema kuwa ataitangaza nchi yake na kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mazingira ili kuweza kuondoa madhara yatokanayo mabadiliko ya tabia nchi.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ofisini kwake. Aidha, amewaomba watanzania kumpa sapoti kubwa kwani anaenda kuiwakilisha nchi na ushindi atakao upata utakuwa ni wa watanzania wote

Wayne Rooney Aumia, Hatarini Kuikosa Arsenal
Video: Bodi ya mikopo yatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu