Mshambuliaji na nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya England Wayne Mark Rooney, hatokua sehemu ya timu itakayocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hispania hii leo.

Rooney amelazimika kuondolewa kwenye kikosi cha England kufuatia mjeraha ya goti yanayomkabili kwa sasa.

Mshambuliaji huyo alicheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Scotland mwishoni mwa juma lililopita ambapo England walichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

Rooney alipatwa na majeraha ya goti akiwa katika mazoezi na wachezaji wenzake hapo jana, na tayari amesharejeshwa Old Trafford kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Hata hivyo kocha wa muda wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate, alikua na matarajio ya kumtumia Rooney kama mchezaji wa akiba katika mchezo wa hii leo, kutokana na mipango aliyojiwekea ya kuwajenga wachezaji chipukizi.

Taarifa za kuumia kwa Wayne Rooney zinaweza kuvuruga mipango ya meneja wa Man Utd Jose Mourinho, kuelekea kwenye mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili, ambapo mashetani wekundu watapambana na Arsenal katika uwanja wa Old Trafford.

Tim Howard Kusubiri Hadi Mwaka 2017
Video: Mrembo Julietha Kabete kuiwakilisha tanzania shindano la Miss afrika