Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa notisi ya siku thelethini (30) kwa wadaiwa wote sugu wawe wameanza kulipa madeni yao kabla ya hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)  Abdul – Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana  na wadaiwa sugu leo Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika  waliokopeshwa na muda wa kulipa madeni hayo umepita bila wao kuwasilisha taarifa zao za kulipia madaeni ya mikopo ya elimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.

Badru ameongeza  kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walibainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao ili waweze kulipa hata hivyo  kati yao ni wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.

Hatua hizo ni pamoja na  kuyatangaza majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajili, wadhamini wao na wadau wengine wenye taarifa za wasugu hao waziwasilishe,kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.

Video: Mrembo Julietha Kabete kuiwakilisha tanzania shindano la Miss afrika
Video: Nape akabidhi Bendera ya Taifa kwa mrembo anaeiwakilisha Tanzania