Waziri wa Habari,  Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye leo amekabidhi bendera ya Taifa kwa mrembo, Julietha Kabete atakae iwakilisha Tanzania katika shindano la Miss Afrika ambalo linatarajiwa kufanyika Novemba 28, nchini Nigeria, shindano hilo linafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Nape amesema ni nafasi ya kipekee Tanzania kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na serikali ya awamu ya tano inataka kuhakikisha mashindano ya ulimbwende yanakuwa na thamani na yenye faida hivyo inamtakia safari njema na ipo nyuma yake kumpa msaada pindi unapohitajika.

“Tunataka mashindano ya Miss Tanzania ambaye anafaidika asiwe namba moja peke yake tumeona hapa huyu alikuwa mtu wa nne na amepata nafasi ya kuwakilisha nchi, tunafahamu mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa yamefungiwa kufanyika ila sasa yamerudi vizuri na tutaendelea kuyaimarisha yawe bora na matarajio ya serikali ni kuona tunakuwa tunafanya vizuri na siku moja hata mshindi wa Miss World atoke Tanzania,” amesema Nape.

Kwa upnde wake mrembo huyo amesema anaomba sapoti kutoka kwa watanzania wote na kuahidi kuwa hato waangusha na ataitangaza vizuri Tanzania “Naomba Watanzania wanisapoti ili nifanikiwe kushinda Miss Afrika ambayo inafanyika Nigeria, ni nafasi ya kipekee ambayo nimepata na nikipata ushindi ni wetu sote,” amesema Julitha

Video: Mtanzania aliyechaguliwa kuiwakilisha Tanzania shindano la Miss Afrika

 

 

 

Video: Bodi ya mikopo yatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu
TB Joshua avunja ukimya kuhusu utabiri wake kuwa Clinton angeshinda Urais