Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano mwandishi wa habari, Erick Kibendera aliyekamatwa Julai 29, 2019 nyumbani kwake maeneo ya Mbweni Jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamtwa baada ya kukataa wito wa polisi ambapo awali aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano, lakini alikaidi kutii wito huo na kusema kwamba,  jeshi la polisi linapomuita mtu kwa hiari na akaacha kutii wito huo, hutumia mbinu ya kumlazimisha atii.

”Baada ya kukamatwa kwa mwandishi huyo, tulisikia taarifa mbalimbali kutoka kwa kada mbalimbali kwenye jamii wakiendelea kusema mwandishi huyo alitekwa niseme kuwa, mwandishi huyo hakutekwa aliitwa, lakini kwa jeuri alikaidi kutii wito huo, sababu pia ya kuitwa ni kuhusiana na utata wa uraia wake, Jeshi linaendelea na upelelezi kwa kushirikiana na maafisa wa uhamiaji”, amesema SACP Mambosasa.

Aidha, Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa, baada ya upelelezi kukamilika jeshi hilo litahakikisha kosa analotuhumiwa nalo mwandishi huyo, linawekwa mezani ili na yeye aweze kuhakikishia kama ni Mtanzania kwa kutoa vielelezo vinavyothibisha uraia wake.
ideo

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 31, 2019
JPM atoa pole kwa familia ya Meja Jenerali Mstaafu Albert Mbowe jijini Dar.