Leo Novemba 11, 2016 viongozi wa Serikali wameungana na Wananchi wa Dar es salaam na Watanzania wote kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samuel Sitta kisha kuelekea Urambo, Tabora ambako mwili wake utaenda kuhufadhiwa.

Akitoa salamu za mwisho za kuaga mwili wa Mzee Sitta, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema ameanza kufahamiana na marehemu Sitta mwaka 2008, na kuanzia hapo amekuwa rafiki yake aliyemsaidia kama baba yake kwani alimsomesha hadi kumaliza chuo na kufanikiwa kusimamia hata harusi yake kama baba.

Makonda amesema amebakia na pengo kubwa ambalo daima litakuwa wazi, lakini Mungu ametwaa kilichochake. Makonda amemshukuru Rais Magufuli pamoja na Rais msataafu Kikwete kwani muda wote wakati uhai wake Mzee Sitta alikuwa akiwasihi watoto wake kushirikiana na viongozi hao kwani ni wema.

Pamoja na hayo, Makonda ametoa ombi kwa Rais Magufuli kuhusu kuwaenzi viongozi waliofanya kazi kubwa katika Taifa letu, kufuatia Makao makuu kuhamishiwa Dodoma, Makonda ameomba kutengenezwa sehemu maalum ya kuhifadhi viongozi na sehemu hiyo iwe kama sehemu ya kumbukumbu na ikiwezekana kuubeba pia na Mwili wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili watu wanapotembelea Makao Makuu ya nchi Dodoma wapate kujifunza historia ya viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki.

Video: Mwili wa Samuel Sitta wawasili Karimjee kwa ajili ya kuagwa

Uenyekiti CUF: Mahakama Kuu yawapa Lipumba, Msajili Siku 7
Video: Mwili wa Samuel Sitta wawasili Karimjee kwa ajili ya kuagwa