Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa limemtia nguvuni mtuhumiwa wa madawa ya kulevya, mfanyabiashara mkazi wa Kizwite katika Manispaa ya Sumbawanga aliyebainika kuyaficha madawa yadhaniwayo kuwa ni heroin katika maua yaliyokuwa yamezunguka nyumba yake.

Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa huo, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amelipongeza jeshi la polisi kwa kufanikiwa kukamata kilo mbili za madawa hayo na lori la scania lililosheheni pombe za viroba lililokuwa likitokea Mbeya na kuingia Rukwa kwa njia za panya.

“Pamoja na kwamba mna-resource ndogo lakini kazi mnayoifanya ni kubwa sana, nawapongeza kwa kitendo hiki na mwendelee kushika kamba hiyo hiyo dhidi ya vita hii ya madawa ya kulevya ambayo si ya jeshi la polisi peke yao bali ni la wananchi wote wa nchi ya Tanzania,” Zelote Stephen alieleza.

Sambamba na hilo Kamanda wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alifafanua kuwa watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na lori aina ya Scania lililosheheni pombe zenye vifungashio vya nailon maarufu pombe za viroba wakitokea Mkoani Mbeya kuelekea Rukwa.

Lori hilo lilikuwa na pombe aina tatu za konyagi,valuer na zanzi cream vikiwa ni jumla ya katoon 364 ndani ya gari no. T. 402 AFC Scania likiwa ni mali ya Kanji Lanji.

Taarifa za Kukamatwa kwa lori hilo zilitolewa na wasamaria wema waliloliona lori hilo likiacha njia kuu na kuingia katika njia za panya katika Kijiji cha Nambogo Kata ya Lwiche, Wilayani Sumbawanga na kuamua kuripoti polisi.

 

Watuhumiwa 11,303 dawa za kulevya wakamatwa
Wema Sepetu amuahidi ‘jambo’ Lema baada ya kutoka gerezani