Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila amesema Congo inatambua umuhimu wa kushirikiana na Tanzania katika biashara na uwekezaji na kwamba amefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Tanzania imezichukua kuboresha huduma katika bandari ya Dar es Salaam ambayo ni tegemeo kwa usafirishaji.

Rais Kabila amesema hayo leo tarehe 04 Oktoba, 2016 wakati akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria katika nchi hizi mbili marafiki na majirani.

Bofya hapa kutazama video

Rais Magufuli afanya mazungumzo Ikulu na rais wa congo DRC
Malinzi: Sitawaacha Serengeti Boys