Rais  wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli leo amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)  Joseph Kabila  ikulu na kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo  viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kidugu katika nchi zao.

Dkt.  Magufuli amemuhakikishia  Rais wa Congo Joseph Kabila  kuwa serikali ya tanzania imeshachukua hatua kadhaa za kuimarisha huduma katika bandari ya Dar es salaam na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kufikia vitatu ili nchi ya congo na zingine ziweze kutumia bandari ya tanzania bila vikwazo.

Aidha Rais Magufuli amesema  tanzania imejiwekea  malengo ya kuhakikisha uchumi wake unakua kwa asilimia 7.2 na kwamba kutokana na hali hiyo,  inawakaribisha wafanyabiashara wa congo kuja  kuwekeza nchini tanzania na wafanyabiashara  wa  tanzania kuwekeza nchini congo

”Mhe Joseph Kabila takwimu zinaonyesha nchi zetu zinafanya biashara kubwa kwani katika mwaka 2009 tulifanya biashara iliyofikia shilingi bilion 23.1 na imekua ikikua mwaka hadi mwaka na hivi sasa tunafanyabiashara yenye thamani ya shilingi bilion393.6 kwa mwaka,     Mimi ningependa kuona sisi ndugu  na majirani tunafanya biashara zaidi, wafanyabiashara wa congo waje tanzania kuwekeza  na serikali yangu itwaunga mkono”Alisema Magufuli.

Rais  Magufuli  pia amezungumzia mikakati ya kuimarisha  mawasiliano ya barabara na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) ambapo tanzania imetenga shilingi Trilion 1 kwaajili ya kuanza ujenzi huo na kwamba hatua hiyo itarahisisha usafirishaji mizigo ya kwenda na kutoka Congo kupitia bandari ya Dar es salaam.

Kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini uganda hadi bandari ya tanga nchini tanzania.rais Magufuli  amesema matarajio kuwa kongo pia ambayo imegundua mafuta katika ziwa albert itatumia bomba hilo kama ambavyo tanzania  inatarajia kulitumia kufuatia tafiti kuonyesha uwepo wa mafuta maeneo ya ziwa Eyasi na Tanganyika.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo Joseph Kabila  amemshukuru rais Magufuli  kwa  mwaliko huo wa kiserikali na amemhakikishia  kuwa Congo itendelea na kuimarisha  zaidi uhusiano na tanzania  kwa kuwa nchi hizi ni majirani na udugu wa tangu enzi za mwalimu nyerere,

”Mhe Rais Magufuli hivi karibuni tutaanza mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu nchini  Congo lengo letu ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani kabla, na baada  ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi desemba”Alisema kabila.

Mhe. Kabila amekubali kuupokea ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Tanzania, Angola na Msumbiji  ambapo ni mwenyekiti wa asasi ya siasa,ulinzi na usalama ya jumuiya ya maendeleo kusini mwa afrika(SADC-Organ Troika) rais magufuli ataituma hivi karibuni kwaajili ya kufuatilia hali ilivyo nchini Congo.

Wafanyakazi wakala wa ufundi na umeme Temesa watakiwa kufanya kazi kwa bidii
Video: Rais wa DRC, Joseph Kabila amhakikishia JPM ushirikiano