Mapenzi ya mashabiki wa jiji la Dublin nchini Ireland yamemzidia Rihanna akiwa jukwaani, hali iliyomfanya aweke kando kikuza sauti na kumwaga chozi zito.

RiRi alijikuta akibubujikwa machozi wakati akiimba wimbo wa ‘Love The Way You Lie’ alioshirikishwa na Emimen, kutokana na namna ambavyo maelfu ya mashibiki walikuwa wakimuonesha mapenzi makubwa baada ya kulipia na kushuhudia show yake ambayo ni sehemu ya ziara ya ‘Anti’.

Ingawa RiRi alishindwa kuendelea kuimba kutokana na machozi yaliyokuwa yakiifuta make up yake taratibu, mashabiki hao walimalizia wimbo huo kwa kuimba wenyewe huku wakiendea kumshangilia.

Angalia kipande cha video hapa:

Trump atumia dola milioni 55 kwenye kampeni za kuwania nafasi ya Urais
Kampeni ya "Let's Move!" Yamuingiza Michelle Obama Snapchat