Aliyekuwa Mwenyekiti wa timu ya simba, Ismail Aden Rage amesema klabu ya Simba imepata pigo kubwa sana kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta kwani alikuwa mwanachama hai na aliyeisaidia sana klabu ya Simba.

Rage amesema pengo aliloliacha mzee Sitta ni kubwa, kwani alikuwa ni mtu wa watu na  mchapakazi.

Amesema kuwa pamoja na mambo mengine anamkumbuka sana wakati alipokuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ambapo alitumia busara kubwa kuweza kuliweka sawa na hatimaye kufika mwisho salama. Bofya hapa kutazama

Mario Balotelli: Ni Wakati Wa Luis Suarez
Live: Uchaguzi wa Rais Marekani 2016, Trump & Clinton