Kuelekea  sikukuu za Chrismass na mwaka mpya, Jeshi la Polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa  makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa tariifa kupitia namba za Makamanda wa Polisi mikoani na namba za bure za 111 na 112.

Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Advera Bulimba amesema hayo mapema leo wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Jeshi la Polisi nchini limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bila kuwepo vitendo vyovyote vya uhalifu.

Kamishina Bulimba amewataka wamiliki wa kumbi za starehe kuzingatia uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo badala ya kuendekeza tamaa ya fedha  kwa kujaza watu kupita kiasi.

Aidha, Wamiliki wa maduka makubwa wametakiwa kufunga Kamera  za CCTV ili kurekodi mienendo ya watu wanaoingia na kutoka katika maduka yao kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali na kuweza kubaini uhalifu na wahalifu kwa haraka.

Video: Mbowe maji ya shingo, Mrithi wa Lubuva NEC afunguka...
Rais Magufuli amteua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi