Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki amesema kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake wako njiani kuanzisha mtaala wa masomo ili rushwa ifundishwe tangu shuleni.

“Napenda kuwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba Serikali ya awamu ya tano haitakubali kuona rushwa ikiota mizizi. Tunaamini wanafunzi wakijengewa uwezo tangu utotoni, watachukia rushwa na hatimaye tutakuwa na Taifa lenye watu waadilifu,” amesema.

Amesema kutokana na zoezi la kupunguza watumishi hewa, hadi kufikia Aprili mwaka huu, Serikali imekwishapokea sh. bilioni 1.2 kwenye akaunti maalum ya TAKUKURU iliyoko HAZINA ambazo zinatokana na makusanyo kutoka kwa waliokuwa watumishi hewa.

Majaliwa apokea taarifa uchunguzi wa Salfa, Ni ya makontena 211 yaliyokuwa bandarini Dar
TFF wakanusha kuitelekeza Serengeti Boys