Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa wabunge wateule wa Chama cha Wananchi (CUF) wataapishwa kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa na Bunge.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa wabunge hao wataapishwa siku ya kuanza shughuli za bunge mapema mwezi ujao.

”Kumekuwa na minong’ono mingi kuhusu wabunge hawa, lakini niwaambie tu kwamba wabunge hawa wataapishwa kama ilivyopangwa, hivyo baada ya kuapishwa tu wataanza kutekeleza majukumu yao,”amesema Ndugai

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 25, 2017
Video: Tukamateni Chadema wote mtuweke rumande- BAVICHA