Wakili wa Kujitegemea, Leonard Manyama amewataka wafanyabiashara kutojihusisha na rushwa pindi wanapokutana na mazingira hayo bali watoe taarifa.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amewataka wafanyabiashara kutoa taarifa mara moja katika vyombo husika ili viweze kuchukua hatua stahiki.

Amesema kuwa ni vyema wafanyabiashara wakajenga uhusiano wa karibu na Takukuru ili watakapokutana na mazingira hayo iwe rahisi kutoa taarifa na kufanikisha kukamatwa kwa wahusika.

”Niwaombe wafanyabiashara waendelee kulipa kodi na wajiepushe na mazingira ya rushwa kwani kutoa rushwa au kupokea ni kosa kisheria, kama kuna mfanyakazi yeyote wa serikali atakuomba rushwa, wasiliana na Takukuru ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa,”amesema Manyama

Video: Mzee Kilomoni hana chake Simba, anapoteza muda-Magori
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 14, 2019

Comments

comments