Wananchi mbalimbali Jijini Dar es salaam wameelezea kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya walimu ambao wamekuwa wakitoa adhabu kali kwa wanafunzi.

Wameyasema hayo jijini Dar es salaam walipokuwa wakizungumza na Dar24 Media katika kipindi cha Sauti Zetu, mbapo wamesema kuwa Serikali itoe adhabu kali kwa walimu wanaokiuka maadili ya kazi zao na kufanya vitendo viozu vya unyanyasaji na kukandamiza haki za watoto.

Aidha, wamesema kuwa kama Serikali isipoingilia kati linaweza kuleta madhara makubwa zaidi ya hapo siku za usoni, kwakuwa wazazi watakosa imani na walimu na hali hiyo itapelekea kusita kuwapeleka watoto wao mashuleni na kutengeneza taifa la watu wasio wasomi.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 1, 2018
Luis Enrique awatema Jordi Alba, Koke