Wapiganaji wa kikosi cha waasi wa ADF kinadaiwa meripotiwa kuwaua watu 12 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, katika shambulio lililofanywa eneo hilo linalokabiliwa na ukosefu wa usalama.

Wapiganaji hao wa Allied Democratic Forces – ADF, walitekeleza mashambulio kwenye kijiji cha Bukokoma, kilichopo jimbo la Kivu Kaskazini katika eneo la Beni, kulingana na mwakilishi wa mashirika ya kiraia Ricardo Rupande.

Kundi la ADF, linalohusishwa wa Islamic State limeripotiwa kutekeleza mashambulio mabaya zaidi mashariki ya DRC ambapo wamewaua maelfu ya raia katika oparesheni zake.

Msimamizi katika eneo la Bukokoma, Katanga Matete alisema wanamgambo hao walikuwa wakifungua milango na kukata vichwa vya watu kwa mapanga na mapanga.

Ditopile awashukia wanaotaka kuiagawa Tanzania
Usiyoyajua kuhusu Wangoni na mgawanyiko wa majina yao