Vikosi vya jeshi nchini Iraq vinasema kuwa vimeteka eneo la mwisho lililokuwa likishikiliwa na wapiganaji wa Islamic State katika mji wa Fallujah.

Jenerali mmoja wa jeshi alisema kuwa jeshi limewatimua wapiganaji kutoka eneo alilolitaja kuwa Golan. Akizunguzma kutoka eneo hilo, alisema kuwa hiyo inamaanisha kuwa vita vya fallujah sasa vimekwisha.

Serikali ilitoa taarifa kama hiyo zaidi ya wiki moja iliyopita ikisema kuwa imeukomboa mji huo. Lakini mapigano ya mitaani bado yalikuwa yakiendelea.

Euro2016: Poland yailaza Switzerland
Vita vyaendelea Sudan Kusini