Kamishna Msaidizi wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto nchini, Faidha Yusuph amewaomba waumini wa Dini ya Kiislamu kujua umuhimu wao katika jamii kwa kukemea vitendo vyote vya ukatili.

ACP Faidha ameyasema hayo wakati akiongea na Waumini hao Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, katika uzinduzi wa Msikiti wa Hemed, ambapo aliambatana na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kilimanjaro, Mrakibu wa Polisi, Asia Matauka.

Amesema, “mnapaswa kutoa mafunzo yaliyomema kwenye nyumba za ibada kwa kuonya, kufundisha, kukemea na kuwakumbusha waumini kutenda matendo mazuri yenye kumpendeza Mungu na kwa jamii inayowazunguka.”

Afande Faidha ameongeza kuwa, Viongozi hao wa Dini pia wanatakiwa kuelewa wao ni walezi na wanadhamana kubwa kuliombea Taifa, ili Vijana wasiwe kinyume na maadili na watoe elimu ya ndoa kabla ya kuwafungisha ili kuepuka migo Gano ya mara kwa mara.

Fanyeni kazi zenye matokeo chanya - Dkt. Biteko
Mafuriko yauwa zaidi ya 30, Serikali yatoa tahadhari