Viongozi wa ngazi za juu mkoani Rukwa akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Mkoa, Zeno Nkoswe wametangaza kujiuzulu nafasi zao kufuatia kutoridhishwa na uteuzi wa wabunge wa viti maalum uliofanywa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa.

Viongozi hao wa Baraza la Chadema wameeleza kuwa mbunge wa viti maalum aliyeteuliwa alikuwa wakala wa TLP na sio Chadema kama walivyodai.

Zeno Nkoswe

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, Zeno Nkoswe

“Aliyeteuliwa mpaka sasa ni yule aliyekuwa wakala wa TLP. Kwahiyo huyo anayeweza asiwe mbunge wa viti maalum wa Chadema akawa mbunge wa viti maalum wa TLP,” alisema Nkoswe na kuongeza kuwa Baraza hilo lilimpendekeza kada wa Chadema Sumbawanga Mjini lakini haikuwa hivyo.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wamesema kuwa uongozi wa ngazi ya Taifa walishindwa kutimiza ahadi zao za kuwalipa mawakala waliosimamia uchaguzi katika maeneo hayo.

Walisema kuwa licha ya kuorodhesha majina ya mawakala hao ambao wamekuwa wakisubiri fedha kutoka makao makuu, fedha hizo hazikuwasilishwa kwao hivyo kuwafanya viongozi hao kugombana na mawakala hao.

FA Kumuadhibu Tena Jose Mourinho?
Masikini Moyes, Kufutwa Kazi Wakati Wowote