Mshambuliaji wa Stand United, Chidiebere Abasirim, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kupata majeraha mabaya katika mchezo wa jana ya ligi kuu soka Tanzania Bara ambao timu yake ilishinda bao moja kwa bila dhidi ya Azam FC Uwanja wa Kambarage Shinyanga.

Chidiebere ambaye ni raia wa Nigeria, aliruka kuwania mpira wa juu na mlinzi wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris ambapo Aggrey Morris alimgonga kwa kiwiko kabla ya kuanguka vibaya .

Nyota huyo alitibiwa Uwanjani kwa dakika nyingi, lakini jitihada ziligonga mwamba na jopo la madaktari wa Stand United wakishirikiana na wa Azam FC walilazimika kumuondoa Uwanjani kumpeleka Hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.

Mapema hii leo wachezaji wa Azam FC, wakiongozwa na kocha mkuu, Seven Hernandez wamemtembelea Chidiebere.

Wachezaji waliofika kumjulia hali mshambuliaji huyo ni Aggrey Morris aliyehusika kwenye tukio, nahodha John Bocco, Bruce Kangwa na David Mwantika.

Naye Kamishina wa mchezo huo, Alfred Lwiza, amemjulia hali Chidiebere aliyekua amelazwa katika Hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga .

Chidiebere anaendelea na matatibabu ambapo baada ya kufikishwa hospitalini hapo alishona sehemu aliyochanika vibaya.

Video: Mambo aliyokemea Mwalimu Nyerere
Nike Yavunja Mkataba Wa Adidas, Kuidhamini Chelsea Hadi 2032