Oktoba 14, 2016 Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anatimiza miaka 17 tangu afariki dunia Oktoba 14, 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas, London, Uingereza  alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa saratani ya damu.

Dar24.com imeongea na Mhandisi Mstaafu, Japhet Mwandimo ambaye aliyefanya kazi enzi za uongozi wa Mwalimu Nyerere ambapo ameelezea kuwa kati ya mambo ambayo Mwalimu ameyakemea ni pamoja na kuondolewa kwa Azimio la Arusha baada ya utawala wake na kusababisha kuporomoka kwa maadili kwa watumishi wa umma, huku baadhi ya viongozi wakjilimbikizia mali.

Mhandisi Mwandimo amesema Mwalimu Nyerere pia alikemea kuuzwa kwa mashirika ya umma ambayo yalikuwa yana zarisha ajira nchini.

Aidha, Mwandimo amemfananisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamiu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika utendaji wa kazi. Bofya hapa kutazama video

Kafulila Akwaa kisiki cha mwisho mahakamani, ubunge wampita kando
Wachezaji Na Kocha Wa Azam FC Wamjulia Hali Chidiebere