Klabu ya Chelsea imethibitisha kuingia mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike baada ya kuvunja mkataba na kampuni ya Adidas.

Kampuni ya Nike imekubali kuidhamini klabu ya Chelsea hadi mwaka 2032 sambamba na kukubali kulipa fedha za kuvunja mkataba wa kampuni ya Adidas ambao ulikua umesaliwa na muda miaka sita.

Taarifa zilizochapishwa katika tovuti ya gazeti la Telegraph la Uingereza zimeelzea kuwa, kampuni ya Nike itoa kiasi Pauni milion 40 kwa lengo la kuvunja mkataba wa mahasimu wao (Adidad) ambao wataendelea kuwa na Chelsea hadi mwishoni mwa msimu huu.

Mbali na kukubali kutoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuvunja mkataba, Nike wamekubali kuilipa Chelsea kiasi cha Pauni milioni 60 kwa kila mwaka, ikiwa ni mara mbili zaidi ya malipo yaliyokua yakifanywa na kampuni ya Adidas.

Mkataba wa klabu ya Chelsea na Nike, utakua na malipo mara tatu zaidi ya ule Manchester City ambao pia wanadhaminiwa na kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Marekani.

Pia mkataba huo unakua na thamani mara mbili zaidi ya mkataba uliosainiwa kati ya klabu ya Arsenal na kampuni ya Puma ya nchini Ujerumani.

Makubaliano mengine ambayo Nike wamekubali kuyabeba kufuatia dili walilosaini na klabu hiyo ya magharibi mwa jijini London, ni kutengeneza vifaa vyote vya michezo kwa ajili ya kikosi cha kwanza, timu za vijana na wanawake pamoja na kubuni mavazi mengine kwa ajili ya mashabiki.

Wachezaji Na Kocha Wa Azam FC Wamjulia Hali Chidiebere
Arsene Wenger Awakatisha Tamaa FC Barcelona