Waziri wa viwanda na biashara nchini Rwanda, Soraya Hakuziyaremye amesema wafanyabiashara wa sokoni watafanya kazi kwa awamu ilikuepusha misongamano kwenye masoko na kudhibiti kusambaa kwa Corona.
Uamuzi huo ni kati ya uamuzi uliofanywa na Baraza la Mawaziri katika kurahisisha zuio la watu kutoka nje na kuhakikisha umbali wa mita moja baina ya wafanyabiashara unazingatiwa huku shughuli nyingine zikiruhusiwa.
”Masoko yatafunguliwa kwa wanaouza bidhaa muhimu ambao watauza kwa awamu, kila awamu kuwa na asilimia 50 ya wafanyabiashara waliosajiliwa” amesema Waziri Mkuu Eduardo Ngirente
Amesema watakaoruhusiwa ni wafanyabiashara kama chakula dawa na bidhaa za usafi lakini bidhaa nyingine kama vifaa vya ujenzi na mavazi hazitaruhusiwa katika masoko.