Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umeitisha maandamano leo Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi, ikiwa ni hatua ya kushinikiza kujiuzuru kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa August 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini.

Tayari rais Uhuru kenyata ametoa onyo kwa wapinzani ambapo amesema kuwa watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi zaraia wa nchi hiyo.

”Endeleeni na maandamano yenu, mkigusa mboga za mama wanaouza barabarani, tuko na nyinyi. Mkigusa maduka ya watu tuko na nyinyi. Lakini kama hamna lingine lolote la kufanya isipokuwa kutembea – tembeeni. Mimi nawaambia hata mukinitukana mpaka asubuhi, haitabadilisha dunia”, alisema Kenyata.

Hata hivyo upinzani umesisitiza kuwa una haki ya kuandamana kwani hata upande Muungano wa Jubilee umeshafanya maandamano kama hayo hivi karibuni  wakitaka majaji wa mahakama ya juu hiyo waondolewe.

Muungano wa NASA unataka jumla ya maafisa 12 wa tume hiyo washtakiwe kwa kutowajibika katika uchaguzi uliobatilishwa wa Agosti 8 huku pia ukitaka mfumo wa teknolojia uliotumiwa wakati wa uchaguzi huo ubadilishwe.

 

 

 

 

Peter aivunjavunja Psquare, ajiita Mr.P
Video: Daktari aeleza Manji alivyo hatarini kupoteza maisha, Sakata la Lissu lilivyomuibua Nyalandu