Baadhi ya wananchi wa Sierra Leone, wamefurahia kupitishwa kwa sheria inayotaka makampuni binafsi na taasisi za serikali kutenga asilimia 30 ya nafasi za ajira kwa ajili ya wanawake.

Kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema hatua hiyo inakusudiwa kuukabili ukosefu wa usawa wa jinsia katika jamii ya nchi hiyo, ambayo inawapendelea zaidi wanaume.

Ni ushindi Kwa Wasichana Nchini Sierra Leone, Serikali pia iliondoa marufuku inayowakataza Wasichana Wajawazito kuhudhuria Shule. Picha ya Equality now.

Rais wa nchi hiyo Julius Maada Bio, amesaini muswaada kuwa sheria ambayo pia inawahakikishia wanawake walau kupata wiki 14 za likizo ya uzazi, kiwango sawa cha mshahara pamoja na fursa za kupata mafunzo.

Katika hotuba yake kwa Taifa, Rais Bio alisema serikali yake itashughulikia ipasavyo ukosefu wa usawa wa kijinsia nchini humo, na kuhakikisha mpango huo unafanikiwa.

Young Africans yarudishwa Gym
Robertinho: Hakuna kama Mgunda, Matola