Klabu ya Ginora ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Municipal de Montilivi iliwaangushia kipigo cha mabao 2-1 Real Madrid katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga uliopigwa jana.
Real Madrid walitangulia kufunga bao la kuongoza lililofungwa na Isco dakika ya 12 kipindi cha kwanza lakini Ginora ambao ni wageni wa La Liga walitoka nyuma na kusawazisha bao hilo kipindi cha pili dakika ya 54 kupitia kwa Cristhian Stuani.
Wakati Madrid wakiwa hawaamini kilichotokea dakika ya 58 Portu struck aliifungia Ginora bao la pili na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Ginora kushinda mabao 2-1.
-
Man City yapunguza kasi kwa Sanchez huku Everton ikimnyemelea
-
Hamilton anyakua taji la nne la Formula 1
-
Bila kisu kikali huwapati wachezaji hawa Uingereza
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana katika La Liga na wamejiwekea historia kwa kuwapiga Real Madrid ambao ni mabigwa watetezi wa La Liga.
Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kushuka mpaka nafasi ya 3 ikiwa imecheza michezo 10 na kuvuna pointi 20 nyuma ya Valencia yenye pointi 24 na Barcelona ambao wapo kileleni mwa La Liga wakiwa na pointi 28.