Wagombea wa kiti cha urais nchini Nigeria, wamemaliza kampeni zao kwa kila mmoja kutoa wito kwa mamlaka kukamatwa kwa mwingine wakishtumiana na kupeana kashfa za zamani za ufisadi.

Wanasiasa hao, ambao waliopendekezwa katika uchaguzi wa urais Bola Tinubu na Atiku Abubakar wote ni matajiri na wamekuwa wakishutumiwa mara kwa mara kwa rushwa, jambo ambalo wamekuwa wakilikanusha vikali huku wenyewe wakishutumiana juu umiliki wa pesa haramu.

Mambo yalivyokuwa wakati wa Kampeni nchini Nigeria. Picha ya PTN.

Zaidi ya Wanigeria milioni 93, wanatarajia kupiga kura ili kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye hatagombea tena uongozi wa Taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika linalokabiliwa na changamoto nyingi, hasa ukosefu wa usalama.

Bola Ahmed Tinubu, mgombea wa chama tawala (APC), anamshutumu Atiku Abubakar, wa upinzani (PDP), kwa kuendesha biashara ya uhalifu na kujenga himaya kwa njia ya udanganyifu kisha kuiba fedha za umma kati ya mwaka 1999 na 2007, wakati akiwa makamu wa rais.

Simba SC Vs Young Africans wasogezwa mbele
Askari 78 waliozuia vitendo vya uhalifu wapewa pongezi