Watu watatu wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kula njama na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika jimbo la Ekiti lililopo kusini magharibi mwa nchi ya Nigeria.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama kuu ya Jimbo la Ekiti, Bamidele Omotoso amesema washitakiwa walitenda kosa hilo Januari 21, 2020 na kuwataja kuwa ni Omotayo Deji (23), Chidiebere Ifeanyin (25) na Bolaji Usman (28) ambao walitiwa hatiani kwa mashitaka manne.

Amesema, “Mei 6, 2019, huko Aba Erinfun, Barabara ya Federal Polytechnic, Ado Ekiti katika Kitengo cha Mahakama cha Ado Ekiti walikula njama ya kutenda kosa la jinai la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuwaibia Ademiloye Stephen, Olokuntoye Temitope na Ajayi Kolade mali zao.”

Aidha ameziorodhesha mali za watu hao watatu zilizoibwa kuwa ni simu, kompyuta mpakato, sandals, chaja za simu na power bank zenye thamani ya Naira 186,000, na wakati wa tukio wezi hao walikuwa wamejihami kwa cutlas na ubao wa mbao.

Bosi Chelsea ajuta kumfuta kazi Tuchel
Balake kuendelea kupeta Simba SC