Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ametoa wito kwa waajiri kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, kwa manufaa ya wafanyakazi pindi watakapopata changamoto za kuumia au kuugua kutokana na kazi.

Ameyasema hayo Mei 22, 2023 katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masalla wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya tathmini za ulemavu uliosababishwa na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari wa mikoa ya kanda ya Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu, Geita na Shinyanga.

Amesema, “ili uweze kunufaika na huduma au mafao yanayotolewa na WCF, ni lazima waajiri wajisajili na kuwasilisha michango ya wafanyakazi waliowaajiri, hivi sasa wafanyakazi wanao uhakika wa kinga na kipato kutokana na majanga yanayosababishwa na ajali, magonjwa na vifo kutokana na kazi kufuatia uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi, WCF.”

Aidha Makalla ameongeza kuwa, uwepo wa Mfuko wa Fidia ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na kazi ikiwemo ya kujenga uchumi na hivyo kuwa na ongezeko kubwa la maeneo ya uzalishaji.

Makambo, Sogne watajwa Kitayosce FC
Robertinho akabidhiwa rungu Simba SC