Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari za Umma, wataanza kufaidika na Serikali ya awamu ya Tano kwa kuondoka na gharama za usafiri wa umma maarufu kama ‘daladala’ jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo njema kwa walimu hao imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Paul Makonda alipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini humo.

Makonda ameeleza kuwa amekuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa vyombo vya usafiri kupitia vyama vya usafirishaji kwa lengo la kuafikiana namna ya kutekeleza mpango huo, na tayari wamefikia muafaka kupitia vikao vyao mbalimbali.

Paul Makonda

“Na muafaka huo ningependa kuwatangazia Walimu na Watanzania, yakwamba sasa kuanzia tarehe 7/3/2016 Walimu wa Shule za msingi na wasekondari watasafiri bure kwenye vyombo vyetu vya usafiri kwa Mkoa wa Dar es salaam,” alisema Makonda.

Alisema kuwa walimu wote wa shule za msingi na sekondari za umma watapewa vitambulisho maalum ili watambulike.

 

Mbowe, Ukawa wavuta pumzi ya mwisho uchaguzi Meya Dar, Zanzibar
Wanajeshi wa Umoja wa Afrika waingia Burundi