Wakandarasi wa kampuni ya Luba, Chuo cha MUST na Ardhi wametakiwa kufika kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida ili wajieleze kwa nini mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo haujamalizika ndani ya wakati, licha ya kulipwa fedha zote na Serikali.

Agizo hilo, limetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma katika hospitali hiyo, huku akiwataka Watendaji kuongeza kasi katika utoaji wa huduma.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel.

Amesema wakandarasi kutoka kampuni ya Luba, Chuo Kikuu cha Sanyansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo Kikuu Ardhi waligoma kufika eneo la ujenzi, licha ya yeye kutoa maelekezo wawepo, ili kujadili changamoto zinazowafanya kushindwa kutekeleza makubaliano ya kumaliza mradi huo kwa wakati.

Aidha, amesema mkandarasi kutoka Luba alitakiwa kumaliza kazi mwezi Julai mwaka 2022 lakini hakutimiza makubaliano hayo licha ya kuongezewa muda mpaka mwezi Novemba mwaka huo huo wa 2022, huku Serikali ikiwa imetimiza jukumu lake la kutoa kiasi chote cha fedha kwa ajili ya mradi huo.

Rais Samia amteuwa Kusaya kuwa Katibu Tawala
Uteuzi Makatibu Tawala, uhamisho wa vituo vya kazi