Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya ameteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari hii leo Machi 16, 2023 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Rais Samia pia amemteua Ally Gugu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Gerald Kusaya.

Kabla ya uteuzi huo, Gugu alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara huku Tixon Nzunda akiteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, akichukua nafasi ya Willy Machumu ambaye amestaafu.

Aidha, Rais amemhamisha Fatuma Manga toka Mkoa wa Dodoma kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida, akichukua nafasi ya Dorothy Mwaluko ambaye amestaafu na Rashid Mchata, ametolewa Mkoa wa Rukwa kwenda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani akichukua nafasi ya Zuwena Jiri ambaye amehamishiwa Mkoa wa Lindi akichukua nafasi ya Ngussa Samike aliyepangiwa kazi nyingine.

Walimu wathaminiwe, walindiwe utu wao: Kairuki
Waliogomea wito wa Naibu Waziri watakiwa kujieleza